MESSI AMEWACHANA LIVE WAANDISHI WA HABARI WA ARGENTINA, AWAONGOZA WACHEZAJI WENZAKE KUGOMA KUFANYA MAHOJIANO NAO
Argentina ni moja ya mataifa yenye wachezaji nguli wa mpira wa miguu na sasa wanajivunia star wao Lionel Messi anayekipiga Klabu ya Barcelona yenye maskani yake Nou Camp.
Lakini katika hali ya kushangaza, Lionel Messi amewaongoza wachezaji wenzie kugoma kuzungumza na waandishi wa habari nchini Argentina baada ya kumaliza mchezo wao na Colombia walioshinda 3 - 0.
Hatua hiyo imekuja baada ya wanahabari wa Argentina kuwa na tabia ya kuwaponda wachezaji wao pale wanapofanya vibaya. Majuzi walipofungwa na Brazil kituo kimoja cha redio kiliripoti kwamba mshambuliaji Ezequiel Lavezzi alivuta bangi akiwa kambini ambapo lavezzi amekanusha vikali na kuahaidi kuchukua hatua dhidi ya kituo hicho.
"Tumepokwa tuhuma nyingi, kukosewa heshina na hatujasema lolote," messi alisema. "Tunajua wengi wenu ambao hamna heshima kwa mchezo huu, lakini kuingilia maisha ya kibinafsi ya mtu mmezidi," Messi aliongeza
Argentina walikosolewa sana baada ya kulazwa 3-0 na Brazil lakini
ushindi wao dhidi ya Colombia umewawezesha kupaa hadi nambari tano na
kwenye nafasi za kushindania kufuzu kwa Kombe la Dunia.
Mataifa
manne yanaomaliza juu kanda ya Amerika Kusini hufuzu moja kwa moja.
Nambari tano hukutana na mpinzani kutoka bara jingine kuamua mshindi.


Leave a Comment