MATATIZO YATOKANAYO NA KUTOA MIMBA

Image result for black pregnant woman

Ivi sasa haswa maeneo ya mijini na vijijini kumekua na wimbi kubwa la wasichana wanatoa mimba kwa kushawishiwa na wapenzi wao, marafiki zao wa wa karibu au wazazi wao kwa kuofia mambo mbali mbali yatakayo weza kuwakatisha safari zao mbali mbali za kimaisha na imeonekana vijana wengi wanadai hawajajipanga katika kuzaa matokeo yake utoa mimba bila kujua madhara ya kitendo hicho na ndio maana nikaoana ni vyemna kushiriki katika page hii kuwaletea madhara yatokanayo na utoaji wa mimba kwa wanawake,  vitendo vya utoaji wa mimba usio salama hasa kwa kutumia madawa yenye kemikali nchi,madawa ya kienyeji na hata watu wasio rasmi na wasio na ujuzi katika utoaji wa mimba hii imezidi sana haswa kwa nchi zinazoendelea ambazo nyingi zipo Africa ikiwemo Tanzania ,wanaotoa mimba sana ni wasichana wadogo ambao wengi wanaanza kutoa mimba wakiwa kuanzia  shule za msingi hadi kwa  wale walioko vyuo vikuu ambao baadae hukumbana na matatizo makubwa kama ifuatavyo

Tatizo kuu la hatari zaidi ni kifo. Imekadiriwa kuwa karibu theluthi moja ya vifo vya kina mama ni kwa sababu ya utoaji wa mimba kwa njia isiyo salama. Kwa kila mwanamke anayekufa, imekadiriwa kuwa wanawake wengine 16 hadi 33 huwa na tatizo baada ya kutoa mimba kwa njia isiyo salama, pamoja na:
  • Hemoreji (kutokwa na damu nyingi)
  • Maambukizi katika kaviti ya pelvisi, au katika mkondo wa damu. (kwa mfano, pepopunda)
  • Kutoboka kwa uterasi (kushona mraruko wa kuta za uterasi kwa kifaa kilicho na ncha kali.
  • Jerahi lililokaribu na ogani katika kaviti ya pelvisi (kwa mfano, uke, kibofu cha mkojo, rektamu na utumbo)
  • Sumu kutokana na dozi ya dawa iliyozidi kipimo chake au mitishamba inayotumiwa kutekeleza utoaji mimba wa kupanga.
Hapo baadaye, mwanamke anaweza kuugua kutokana na maumivu ya pelvisi yanayoendelea kwa muda mrefu (yanayojirudia), hasa wakati wa hedhi, mimba kutoka pekee yake unaojirudia au utasa.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.