MANCHESTER UNITED KUMWONGEZEA IBRAHIMOVIC MKATABA WA MWAKA MMOJA
Manchester United imesema kuwa
itamuongezea mkataba wa mwaka mmoja mshambuliaji wake Zlatan
Ibrahimovic kulingana na meneja Jose Mourinho.
Mchezaji huyo wa
Sweden mwenye umri wa miaka 35 alihamia Old Trafford katika uhamisho wa
bure katika msimu huu akiwa na uwezo wa kuongeza mkataba huo kwa
msimu wa pili. Amefunga mabao 17 katika michuano yote msimu huu.
Mourinho alisema: Tutaanda mpango wa kuongeza mkataba wake kwa mwaka mwengine .Baadaye anaweza kufanya atakacho.
Ibrahimoviv alisema: Najihisi vyema, ikiwa nitaendelea itakuwa mwaka mwengine.
Ibrahimovic
aliyefunga mabao 62 katika mechi 116 akiichezea Sweden kabla ya
kustaafu katika soka ya kimataifa mnamo mwezi Juni ,alikihama klabu cha
PSG mwishoni ma msimu uliopita


Leave a Comment