MAJINA YA WATAKAOGOMBANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA KUTOKA BBC YATAJWA, TIZAMA WASIFU WA WACHEZAJI HAO
Wachezaji watano watakaoshindania Tuzo ya BBC ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka 2016 wametangazwa.
Wachezaji hao ni Pierre-Emerick Aubameyang, Andre Ayew, Riyad Mahrez, Sadio Mane and Yaya Toure.
Wachezaji hao watano walitangazwa wakati wa kipindi maalum cha moja kwa moja runingani Jumamosi.
Mshindi
atachaguliwa na mashabiki wa soka ya Afrika kutoka kila kona ya dunia.
Mashabiki wana hadi saa 18:00 GMT tarehe 28 Novemba kumpigia kura
mchezaji wanayempenda.
Mnamo Jumatatu, 12 Desemba, mshindi wa tuzo
hiyo atatangazwa moja kwa moja kwenye runinga ya BBC Focus on Africa
pamoja na redio, kuanzia saa 17:35.
Tovuti ya SIRI ZA JAMII pia zitachapisha habari za mshindi.
Aubameyang
ameorodheshwa kwa mwaka wanne, mshindi wa mwaka 2011 pia
ameorodheshwa kwa mwaka wa nne, Mahrez ndiye mchezaji pekee ambaye
hajawahi kuorodheshwa kushindania, Mane alishindania mara ya kwanza
mwaka jana naye mshindi mara mbili. Toure ameorodheshwa kwa mwaka wa
nane.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Aubameyang amekuwa na kipindi cha
kufana sana mwaka 2016, amefunga mabao 26 (kufikia wakati wa kuandika
makala hii) katika klabu yake ya Borussia Dortmund nchini Ujerumani
Alikuwa
mchezaji wa kwanza kutoka Afrika kutawazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka
wa Bundesliga, raia wa kwanza wa Gabon kushinda Tuzo ya Shirikisho la
Soka Afrika ya mchezaji bora wa mwaka Afrika, na ameorodheshwa miongoni
mwa wachezaji wanaoshindania tuzo ya mchezaji bora duniani mwaka 2016,
tuzo ya Ballon d'Or.
Mwezi Agosti West Ham walivunja rekodi yao ya kununua wachezaji,
walipolipa Swansea £20.5m kumchukua nyota wa Ghana Ayew, ishara tosha ya
kiwango kizuri cha kiungo huyo wa kati mwaka mmoja uliopita.
Ayew
amekuwa akicheza vyema sana, na magoli 12 aliyoyafunga msimu wa 2015/16
mechi 35 alizochezea Swansea, ulimfanya kuitwa mchezaji bora mgeni wa
klabu hiyo wakati wa tuzo za mwisho wa msimu mwezi Mei.
Mchezaji mwingine wa Ligi Kuu ya England anayechezea Leicester City,
Mahrez kutoka Algeria alifana sana na kutekeleza mchango mkubwa kwa
klabu yake - ambayo uwezekano wake wa kushinda mwanzo wa msimu ulikuwa
5,000-1- na kuiwezesha kushinda ligi mara ya kwanza.
Mahrez
alifunga mabao 17 ligini msimu wa 2015/16 na alichaguliwa na Chama cha
Wachezaji wa Kulipwa Uingereza kuwa Mchezaji Bora wa mwaka - Mwafrika wa
kwanza kushinda tuzo hiyo.
Kadhalika, aling'aa na kusaidia Algeria kufuzu kwa Kombe la Taifa Bingwa Afrika 2017.
Mshambuliaji wa kimataifa kutoka Senegal Mane aliibuka mchezaji ghali
zaidi katika historia ya soka Afrika aliojiunga na Liverpool kwa £34m
majira ya joto mwaka huu.
Uchezaji wake ulidhihirika mara moja
uwanjani Anfield, ambapo aliwafungia Liverpool mabao sita na kusaidia
ufungaji wa mengine manne katika mechi 11. Ni kama aliendeleza kutoka
alipoachia Southampton, ambapo alikuwa amefunga mabao manane ligini
akichezea Saints mwaka 2016, ikiwa ni pamoja na mabao matatu
aliyoyafunga dhidi ya mabingwa wa wakati huo Manchester City.
Toure alijishindia kombe jingine mwaka 2016, kombe lake la 17 katika
maisha yake ya uchezaji, aliposhinda Kombe la Ligi Uingereza akiwa na
Manchester City, ambapo alifunga penalti ya ushindi wakati wa matuta
dhidi ya Liverpool kwenye fainali.
Huu ulikuwa mwaka ambao kigogo
huyu wa safu ya kati kutoka Ivory Coast, ambaye sasa ana miaka 33,
alistaafu soka ya kimataifa baada ya ufanisi mkubwa lakini bado
akajidhihirisha kwamba hajaishiwa na nguvu ya kucheza na kujumuishwa
kwenye orodha hii kwa mwaka mwingine kunatilia mkazo hili.







Leave a Comment