MAANDAMANO MAKUBWA YAFANYIKA KUPINGA USHINDI WA TRUMP MAREKANI


Kumekuwa na maandamano ya kupinga ushindi wa Donald Trump kutoka katika miji mbalimbali nchini Marekani.
Maelfu ya raia kwa sasa wamekusanyika nje ya mnara maarufu kama Trump Tower mjini New york wakipaza sauti zao kuhusu sera za uhamiaji,mapenzi ya jinsia moja na haki ya uzazi yanayopingwa na Donald Trump.
Wanasema hata dunia ina wasiwasi juu ya ushindi wa urais.
Aidha aliyekuwa mpinzani wa Donald Trump, Mama Hilary Clinton amewaambia wamarekani katika Hotuba yake kwamba Trump anastahili nafasi ya kuongoza.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.