KWA MARA INGINE TENA, GARETH BALE ACHUKUA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA WA WALES
Winga wa timu ya taifa ya Wales ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Wales kwa mara ya nne mfululizo.
Gareth Bale na Joe Allen wakiwa na timu ya taifa ya Wales
Bale mwenye umri wa miaka 27 kwa ujumla ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa nchi yake kwa mara sita.
Kiungo
wa Stoke City Joe Allen ametwaa tuzo mbili tuzo ya wachezaji na tuzo
ya washabiki, huku mchezaji wa timu ya Exeter City, Ethan Ampadu mwenye
umri wa miaka 16 akitwaa tuzo ya chipukizi bora.
Ethan Ampadu
Wachezaji wengine waliopata tuzo hizo ni kiungo Aaron Ramsey
aliyepata tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya ulaya ya mwaka 2016.
Mshambuliaji
Robson-Kanu akipata tuzo ya goli bora la michuano ya ulaya ya mwaka
2016, goli lililompa tuzo ni la mchezo wa robo fainali dhidi ya
Ubelgiji.
Natasha Harding,amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa Wanawake



Leave a Comment