KUELEKEA MCHEZO WA YANGA NA PRISONS - HIZI NI REKODI ZINAZOIEBA YANGA KILA ANAPOKUTANA NA PRISONS
Jumapili November 6 kutakuwa na mchezo wa kuvutia kwenye uwanja wa
Sokoine utakaozikutanisha Tanzania Prisons na Yanga katika mwendelezo wa
ligi kuu Tanzania bara.
Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu mbaya ya
kupoteza mchezo wake wa mwisho kwenye uwanja wa Sokoine ilipochezea
kichapo kutoka kwa ndugu wa Prisons timu ya halmashauri ya jiji la
Mbeya, Mbeya City.
Kwa upande wa Tanzania Prisons, nao walikutana na kipigo cha goli 1-0
ugenini dhidi ya Ndanda kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini
Mtwara.
Hapa kuna rekodi na mambo muhimu yanayozihusu timu hizo kabla ya mchezo wao utakaochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Tanzania Prisons vs Yanga head to head
06/11/16 Tanzania Prisons ?? Yanga
03/02/16 Tanzania Prisons 2-2 Yanga
16/09/15 Yanga 3-0 Tanzania Prisons
18/02/15 Tanzania 0-3 Yanga
28/09/14 Yanga 2-1 Tanzania prisons
26/03/14 Yanga 5-0 Tanzania Prisons
18/09/ 13 Tanzania Prisons 1-1 Yanga
Mechi 8 zilizopita
Yanga
Imeshinda mechi 5, nne kati ya hizo imeshinda kwenye uwanja wa
nyumbani mchezo mmoja imeshinda ugenini huku mechi tatu zikiwa ni sare.
Yanga haijapoteza hata mchezo mmoja dhidi ya Tanzania Prisons katika
mechi 8 zilizopita.
Wakali wa Jangwani wamefunga magoli 19, magoli 13 kati ya hayo
yamefungwa kwenye uwanja wao wa nyumbani huku magoli 6 yakifungwa kwenye
uwanja wa ugenini. Wameruhusu magoli 5, mawi kati ya hayo wamefungwa
kwenye uwanja wao wa nyumbani lakini magoli matatu wamefungwa kwenye
uwanja wa ugenini.
Katika michezo nane iliyopita, Yanga imefanikiwa kuchukua pointi 18
kwa Tanzania Prisons. Pointi 12 wamezipata kwenye uwanja wa nyumbani na
pointi 6 walifanikiwa kuzipata kwenye uwanja wa ugenini.
Tanzania Prisons
Mechi 8 ambazo Tanzania Prisons imecheza dhidi ya Yanga haijafanikiwa
kutoka na ushindi. Imefungwa mara 5 na kupata sare 3. Katika mechi 5
ambazo wamepoteza, mechi nne wamefungwa ugenini, mechi moja kwenye
uwanja wao wa nyumbani, sare zote wamezipata kwenye uwanja wao wa
nyumbani.
Wamefungwa magoli 19, magoli 6 wamefungwa kwenye uwanja wa nyumbani huku magoli 13 wakiyaruhusu ugenini.
Mechi 6 zilizopita ndani ya VPL msimu huu
Tanzania Prisons
02/11/16 Ndanda 1-0 Tanzania prisons
29/10/16 African Lyon 1-1 Tanzania Prisons
23/10/16 Mbao 1-1 Tanzania Prisons
19/10/16 Tanzania Prisons 2-1 Stand United
15/10/16 Mtibwa Sugar 0-0 Tanzania Prisons
12/10/16 Ruvu Stars 0-0 Tanzania Prisons
Yanga
02/11/16 Mbeya City 2-1 Yanga
29/10/16 Yanga 3-0 Mbao
26/10/16 Yanga 4-0 Ruvu Stars
22/10/16 Kagera Sugar 2-6 Yanga
19/10/16 Toto Africans 0-2 Yanga
16/10/16 Azam 0-0 Yanga
Nafasi kwenye ligi msimu huu
Yanga
Ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 27 baada ya
kucheza michezo 13 pointi nane nyuma ya vinara wa ligi Simba.
Tanzania Prisons
Yenyewe ipo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi 13
hadi sasa pointi 11 nyuma ya Yanga huku wakiwa nyuma kwa pointi 19 dhidi
ya Simba wanaoongoza ligi hiyo.


Leave a Comment