KOREA KUSINI : RAIA WAANDAMANA KUTAKA RAIS WA KOREA KUSINI AJIUZULU
Kwa wikendi ya tatu mfululizo wananchi wa Korea Kusini waliyojawa na
ghadhabu wameamua kumiminika katika barabara za mji mkuu wa Seoul
kumtaka rais wa taifa hilo Park Guen Hye kujiuzulu.
Mandamano ya leo yanatarajiwa kuwa makubwa zaidi. Viongozi wa maandamano hayo wanasema mamilioni ya watu watashiriki.
Maelfu
ya maafisa wa polisi wa kukabiliana na ghasia,wamepelekwa katika mji
mkuu wa Seoul kukabiliana na waandamanaji hao wanaopinga serikali kufika
ikulu ya rais.
Rais Park Guen Hye, anatuhumiwa kwa kuwa na uhusiano wa karibu na
Choi Soon-sil, anayekabiliwa na shtaka la kujaribu kuibia serikali fedha
nyingi kupitia kampuni kadhaa za taifa hilo.
Bi Choi amekamatwa na kushtakiwa kwa ubadhirifu wa pesa za umma na utumizi mbaya wa mamlaka.
Maafisa kadhaa wanaohudumu katika ofisi ya Rais Guen Hye pia wanachunguzwa dhidi ya sakata hiyo.
Rais wa Korea Kusini Park Guen Hye



Leave a Comment