KIONGOZI NGULI WA CUBA, FIDEL CASTRO AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 90
Fidel Castro, kiongozi wa zamani wa
Cuba aliyeongoza mapinduzi ya Kikomunisti, amefariki dunia akiwa na umri
wa miaka 90, kakake ametangaza.
"Amiri jeshi mkuu wa mapinduzi ya
Cuba alifariki dunia mwendo wa saa 22:29 usiku huu (03:29 GMT
Jumamosi)," Rais Raul Castro ametangaza.
Fidel Castro alitawala Cuba kama taifa la chama kimoja kwa karibu miaka 50 kabla ya kakake Raul kuchukua hatamu 2008.
Wafuasi wake walisema alikuwa ameirejesha Cuba kwa wananchi.
Lakini alituhumiwa pia kwa kuwakandamiza wapinzani.
Chini ya uongozi wa Fidel Castro, Cuba ilikuwa na uhusiano maalum na Afrika.
Katika
miaka ya 1970 na 80, maelfu ya madaktari na walimu walikwenda Afrika na
idadi sawa ya askari wa Cuba walipelekwa huko kuingilia kati migogoro
na wakala wa vita baridi hasa nchini Angola.
Mwezi Aprili, Fidel Castro alitoa hotuba nadra siku ya mwisho ya mkutano mkuu wa Chama cha Kikomunisti.
Alikiri kwamba alikuwa amezeeka sana lakini akasema maadili ya kikomunisti kwa Cuba bado yana maana na kwamba raia "watashinda".
"Karibuni
nitatimiza miaka 90," rais huyo wa zamani alisema, na kuongeza kwamba
ni "jambo ambalo sikuwahi kulifikiria lingetimia".
"Hivi karibuni, nitakuwa kama hao wengine wote, "kwetu sote, wakati wetu lazima utafika"", Castro alisema.
Castro alikabidhi madaraka kwa muda kwa kakake mwaka 2006 alipokuwa anaugua maradhi ya utumbo.
Raul Castro alikabidhiwa rasmi madaraka ya urais miaka miwili baadaye.
Fidel Castro na Che Guevarra enzi za uhai wao



Leave a Comment