KINDA WA JUVE ALIYEZALIWA MWAKA 2000 AWEKA REKODI KWENYE LIGI YA ITALY
Moise Kean amekuwa mchezaji wa kwanza aliyezaliwa mwaka 2000 kucheza
kwenye moja ya ligi nne bora barani Ulaya baada ya kuingia kwenye mchezo
wa Juventus dhidi ya Pescara.
Kinda huyo wa miaka 16 anayekipiga timu ya taifa ya Under-17 ya Italy
alitokea benchi kuchukua nafasi ya Mario Mandzukic zikiwa zimesalia
dakika sita pambano kumalizika.
Kijana huyo aliyezaliwa February 28, 2000, anafanishwa na Mario
Balotelli kutokana na uwezo wake uwanjani ameshatajwa mara tano kukaa
kwenye benchi la wachezaji wa akiba na kocha Massimiliano Allegri katika
mechi za Serie A na mara mbili katika mechi za Champions League.
Juventus sasa wako mbele kwa pointi saba dhidi ya AS Roma walio nafasi ya pili ambao watacheza na Atalanta Jumapili hii.
Sami Khedira, Mandzukic pamoja na Hernanes walifunga magoli ya Juve
na kuifanya timu hiyo kuufukuzia ubingwa wa Serie A kwa mara ya sita
mfululizo


Leave a Comment