JOSEPH KABILA HATOGOMBEA NAFASI YA URAIS TENA
Rais wa Jamhuri ya Demokrasi ya
Congo Joseph Kabila, amewahakikishia raia wake kwamba ataheshimu katiba
ya nchi na kwamba hatawania urais katika Uchaguzi mkuu ujao.
Akilihutubia bunge la taifa, Kabila ameomba kuwepo amani na utulivu.
"Kwa
wale ambao wanaingilia kati maisha yangu ya siasa kila siku, nina sema
asante lakini wafahamu ya kwamba Jahmuri ya Kidemorisia ya Congo ni
nchi inayoongozwa na katiba hatujakiuka katiba na tutaendelea
kuiheshimu. Kwa mda huu kilicho muhimu ni kuangalia maisha ya
wakongomani" Alisema Kabila.
Jana waziri mkuu Augustina Matata Ponyoa alijiuzulu kutoa nafasi wadhifa huo kuchukuliwa na upinzani kwenye utawala wa mpito.
Hatua hii ni ya kutuliza msukosuko wa kisiasa nchini DRC baada ya vyama vikuu vya kisiasa kususia mazungumzo ya kitaifa.


Leave a Comment