ISRAEL: MOTO MKUBWA UMEIBUKA, WAZIRI MKUU ASEMA NI NJAMA ZA MAGAIDI
Waziri mkuu wa Israel Benjamin
Netanyahu amesema kuwa moto mkubwa ulioenea Magharibi mwa nchi hiyo
huenda umesababishwa makusudi na yawezekana likawa ni tukio la kigaidi.
Akizungumza
na wananchi katika mji wa Haifa ampapo zaidi ya maelfu ya wananchi
waliondolewa kwenye makazi yao, amesema ni moja kati ya milipuko sita ya
moto iliyowahi kutokea siku chache zilizopita ambapo maelfu ya makazi
yameharibiwa kwa moto.
Moto huo unachochewa na hali ya ukavu unaosababisha moto kuenea haraka.
Nchi kadhaa zimetuma vikosi vya ndege vya zimamoto kusaidia kuzima moto huo ulionea pakubwa kwa muda mfupi.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu



Leave a Comment