INDIA: WAZIRI MWENYE NYUMBA YENYE CHOO KINACHOZUIA RISASI, SOMA WALICHOANDIKA RAIA WA INDIA MITANDAONI BAADA YA WAZIRI WAO KUMILIKI NYUMBA HIYO


Waziri mkuu wa jimbo la Telangana nchini India amezua hisia baada ya kuhamia katika nyumba mpya inayogharimu walipa kodi dola milioni 7.3.
Jumba hilo lina ukubwa wa mita 9,000 mraba katika mji wa Hyderabad.
Nyumba hiyo ina vyoo vilivyo na uwezo wa kukinga risasi kuingia, ukumbi ulio na viti 250 na eneo la mikutano linaloweza kuingiza watu 500.


Jumba hilo lilibarikiwa na mshauri wa maswala ya kidini wa waziri huyo huku choo hicho kinachoweza kuzuia risasi kuingia kikifanyiwa masikhara.
Waziri mkuu K Chandrashekhar Rao alihamia katika jumba hilo siku ya Alhamisi baada ya msururu wa matambiko ya kidini yalioongozwa na mshauri huyo wa maswala ya kidini Chinna Jeeyar Swamy. 

 Matambiko makubwa yalifanyika wakati wa kuhamia kwenye nyumba hiyo
Bw Swamy pia aliketi katika kiti rasmi cha bw Rao ili kukibariki.
Jumba hilo kwa jina Pragathi Bhavan lilijengwa kwa ushirikiano wa vaastu.
 Hizi ni baadhi ya Tweets walizoandika wananchi wa India baada ya Waziri huyo kuhamia kwenye hekalu lake.



No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.