INDIA: MWANASIASA AGHARAMIA HARUSI YA BINTI YAKE KWA DOLA MILLIONI 74, WANANCHI WAILALAMIKIA SERIKALI
Harusi moja ya kifahari nchini India
ya binti wa mwanasiasa mmoja imezua ghadhabu ya umma, kutokana na
gharama yake wakati mamilioni ya raia wakiwa maskini.
Harusi hiyo
iliyofanyika kwa siku tano ilifadhiliwa na mwekezaji mashuhuri ambae pia
alikua Waziri katika jimbo moja India, G Janardhana Reddy.
Mwanasiasa huyo aliandaa kwa heshima ya binti yake aliyekua bibi harusi bi, Brahmani na iligharimu dola milioni 74.
Kadi za mwaliko zilirembeshwa kwa dhahabu, huku wageni wakitumbuizwa na wasanii kutoka Bollywood.
Watu wengi wamelalamikia harusi hiyo kama kejeli kwa masikini na onyesho la utajiri.
Ilifanyika
wakati serikali ya India ilipotangaza kuondoa sarafu ya rupee ya 500 na
1000 kama hatua ya kuchunguza mali iliyopatikana kwa njia isiyo
halali.
Mamilioni ya raia wa India wamekua wakipanga foleni
kubadilisha sarafu zao na wengi wamelalamikia hatua ya serikali.Harusi
nchini India huwa za kifahari na gharama zote hulipiwa kwa pesa taslimu.
Bwana
Reddy ametetea heshima yake kwa bintiye akisema ilimbidi kuuza baadhi
ya mali zake zilizoko, Bangalore na Singapore ili kugharamia harusi
hiyo. Aidha amesema malipo yote yalifanyika miezi sita kabla ya harusi
kufanywa.
Licha ya kujitetea , raia wengi wamelalamikia kwenye mitandao ya kijamii.
Baadhi ya wakosoaji wa serikali wametaka chama tawala cha Waziri Mkuu Narendra Modi cha 'Bharatiya Janata Party' {BJP}, kuwachunguza wanachama wake dhidi ya ufisadi.
Bwana Reddy aliwahi kufungwa jela miaka mitatu kwa makosa ya ufisadi. Aliachiwa huru kwa dhamana mwaka uliopita. Hekalu ambapo harusi hiyo iliandaliwa zilirembeshwa kwa dhahabu na michoro maalum iliyotungwa na waandaa filamu kutoka Bollywood.
Kuna magari maalum ya kifahari pia iliyowasafirisha wageni waalikwa

Leave a Comment