HILARY CLINTON : "FBI NDIYO CHANZO CHA MIMI KUSHINDWA UCHAGUZI MKUU MAREKANI"
Aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais
wa Marekani kwa tiketi ya Chama cha Democratic Hillary Clinton, amesema
kwamba kushindwa kwake ghafla katika uchaguzi uliyopita, kulichangiwa
pakubwa na hatua ya mkurugenzi wa shirika la kijasusi la Marekani FBI,
James Comey kutangaza uchunguzi mpya wa sakata ya barua pepe dhidi yake
muda mfupi kabla ya uchaguzi.
Bi Clinton amewaambia wafadhili wa
chama chake kwamba hatua ya Comey ilisambaratisha kampeini yake, licha
ya uchunguzi huo kutompata na hatia.
Mwandishi wa BBC nchini
Marekani hata hivyo amesema wengi wanahisi kuna msururu wa sababu
zilizomfanya Donald Trump kumshinda katika uchaguzi huo.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la kijasusi nchini Marekani FBI James Comey
Maelfu ya waandamanaji walifanya maandamano kwa siku nne mfululizo dhidi ya rais mteule Donald Trump.
Mjini New York ,maafisa wa polisi waliwazuia waandamanaji waliojaribu kukaribia bustani ya Union Square.
Wengine walielekea katika jumba la Trump Tower, nyumbani kwa bwana Trump pamoja na makao makuu ya biashara za Trump.
Leave a Comment