HILARY CLINTON AELEZEA MACHUNGU ALIYONAYO BAADA YA KUSHINDWA URAIS KWENYE UCHAGUZI MKUU MAREKANI


Mgombea urais wa chama cha Democratic Hillary Clinton ameelezea masikitiko yake alipojitokeza hadharani mara ya kwanza tangu ashindwe kwenye uchaguzi wa rais nchini Marekani na Donald Trump wa chama cha Republican.
Bi Clinton, akihutubia mjini Washington DC amesema alikuwa hataki kutoka nyumbani tena.
Ameliambia shirika la kuwasaidia watoto wasiojiweza kwamba uchaguzi huo umewafanya Wamarekani wengi kutafakari.
Bi Clinton aliongoza kwa wingi wa kura za kawaida lakini akashindwa kinyang'anyiro cha urais kupitia kura za wajumbe, ambazo ndizo huamua mshidni wa urais.
"Sasa, nitakiri kwamba kuja kwangu hapa halikuwa jambo rahisi," alisema alipokuwa akitunukiwa heshima na wakfu wa Children's Defense Fund.
"Kuna nyakati kadhaa wiki hiyo moja iliyopita ambapo nilitaka kujikunyata tu nikiwa na kitabu kizuri na nisiwahi kutoka nje ya nyumba tena."
Aliendelea: "Ninajua wengi wengu mmevunjwa moyo sana na matokeo ya uchaguzi. Hata mimi, pia, zaidi kushinda ninavyoweza kueleza.
"Ninajua si jambo rahisi. Najua wiki moja iliyopita, watu wengi wamekuwa wakijiuliza iwapo Marekani ni nchi ambayo tumekuwa tukiamini ndiyo.


No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.