HECTOR BELLERIN ATIA SAINI KWENYE MKATABA MPYA NA ARSENAL
Beki wa kulia wa Arsenal kutoka
Uhispania Hector Bellerin ametia saini mkataba mpya wa muda mrefu katika
klabu hiyo inayocheza Ligi ya Premia.
Bellerin, 21, alijiunga na Arsenal mwaka 2011 na amekuwa mmoja wa wachezaji wa kikosi cha kwanza.
Alitia
saini mkataba mwingine wa muda mrefu Julai 2015 lakini amekuwa
akihusishwa na kuhamia klabu kadha, ikiwemo Barcelona alikotoka na
Manchester City.
Arsenal haijatoa maelezo zaidi kuhusu mkataba wake mpya alioutia saini leo Jumatatu
"Nimekuwa hapa muda mrefu, nahisi kama hapa ni nyumbani na hili ndilo jambo bora zaidi kufanya," Bellerin amesema.
"Nina furaha, tena zaidi, kuwa Gunner kwa miaka mingi zaidi."
Bellerin amecheza mechi 67 za ligi kuu, zikiwemo 11 msimu huu.
Hata hivyo atakaa nje wiki nne baada ya kuumia akicheza dhidi ya Tottenham Hotspur


Leave a Comment