HATIMAYE YAYA TOURE AOMBA RADHI MAN CITY
Kiungo wa Manchester City na timu ya taifa Ivory Coast Yaya Toure mwenye umri wa miaka 33, ameomba radhi kwa uongozi wa Manchester City kupitia ukurasa wake wa Facebook.
Kiungo huyo amesalimu amri baada ya kutochezeshwa kwa muda na kocha wa klabu hiyo Pep Guardiola ambaye alinukuliwa kuwa Yaya Toure hatocheza tena kama hatoomba msamaha.
Kupitia taarifa kwenye ukurasa wake wa Facebook, amesema: "Naomba
radhi - kwa niaba yangu na watu wanaoniwakilisha - wasimamizi wa timu na
wote wanaofanya kazi katika klabu hii kwa sababu ya sitofahamu
zilizotokea awali.
"Matamshi hayo hayawakilishi msimamo wangu kuhusu klabu au watu wanaofanya kazi katika klabu hii."
Wiki iliyopita, Guardiola aliambia wanahabari kwamba anamuhitaji
Toure lakini bado anasubiri kuombwa msamaha na ajenti wa mchezaji huyo
Dimitry Seluk.
Toure, 33, ameshiriki katika mechi moja kati ya mechi nane walizozicheza Manchester City msimu huu.
Baada
ya kuachwa nje ya Guardiola kikosi cha wachezaji watakaocheza Ligi ya
Klabu Bingwa Ulaya, Seluk alisema kuwa kiungo huyo wa kati
''alifedheheshwa'' na kwamba Gurdiola anafaa kumuomba msamaha iwapo City
haitashinda kinyang'anyiro hicho.
Ni hapo ambapo Guardiola alijibu na kusema Toure hangecheza tena hadi ajenti huyo aombe msamaha.
''Sitakubali
kama kocha kila ajenti, kwenda kwa vyombo vya habari kuwasilisha
malalamiko yao iwapo mchezaji wake hajashirikishwa kwenye kikosi,"
Guardiola alisema.
Guardiol alikuwa kocha mkuu Barcelona Toure alipouzwa kwa Manchester City mwaka 2010.


Leave a Comment