FIFA WATOA VIWANGO VIPYA VYA UBORA DUNIANI, ARGENTINA YASHIKA NAMBA MOJA
Shirikisho la kandanda ulimwenguni
(FIFA) limetoa orodha ya viwango bora vya soka ,ambapo mpaka sasa kwa
upande wa bara la Ulaya na America Argentina bado ndio taifa bora duniani kwa
mujibu wa viwango vya ubora duniani iliyotolewa Ijumaa.
Brazil, chini ya kocha wao mpya, inakuja moto na kuinyemelea kwa kasi.
Kwa
upande wa Afrika Senegal ndio vinara na ipo nafasi ya 33
ulimwenguni , huku wakifuatwa na Ivory Coast katika nafasi ya pili
ambapo wanafungana na Tunisia kwenye Nafasi hiyo na nafasi ya 36 ni
Misri na wapo nafasi ya 34 ulimwenguni.
Nafasi kumi bora Argentina, Brazil, Ujerumani, Chile, Ubelgiji, Colombia, Ufaransa , Ureno, Uruguay, Hispania.
Orodha nyengine ya Fifa ya ubora duniani itatolewa Disemba 22
Leave a Comment