DONALD TRUMP: "WATAKAOTEULIWA KATIKA NAFASI MBALI MBALI SERIKALINI NAWAJUA MIMI NA SI VINGINEVYO"
Rais mteule wa Marekani Donald Trump
ametetea utaratibu wa mpito nchini humo na kusema hakuna mzozo kinyume
na inavyotangazwa kwenye vyombo vya habari.
Bw Trump ameandika
kwenye Twitter kwamba shughuli ya kuwachagua mawaziri wake inaendelea
"kwa mpango" na kwamba ni yeye pekee awajuaye watu watakaoteuliwa.
Mbuneg wa zamani, Mike Rodgers, aliyekuwa akisimamia masuala ya usalama wa taifa katika kundi la mpito amejiuzulu.
Taarifa katika vyombo vya habari zimedokeza kwamba kuna mzozo mkali
miongoni mwa maafisa wanaosimamia shughuli ya mpito upande wa Bw Trump,
ambao makao makuu yao yamo katika jumba la Trump Tower, New York.
Meya
wa zamani wa New York, Rudolph Giuliani, ambaye anatarajiwa kupewa
wadhifa mkuu, amesema shughuli ya mpito huwa ngumu na ni kawaida
kukumbwa na matatizo madogo hapa na pale.
Bw Trump ataapishwa kuwa rais 20 Januari mwaka 2017


Leave a Comment