DONALD TRUMP AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KWENYE MGAHAWA MMOJA NCHINI MAREKANI NA KUSEMA MACHACHE


Rais mteule wa Marekani Donald Trump aliwashangaza wateja, na wanahabari wanaofuatilia safari zake, baada ya kujitokeza kwa kushtukiza katika mgahawa mmoja New York.
Wanahabari waliopewa kazi ya kufuatilia safari zake walibaki kushangaa kwani walikuwa wameelezwa kwamba angesalia nyumbani jioni hiyo.
Lakini badala yake, aliandamana na kundi ndogo la maafisa hadi kwenye mgawaha wa 21 Club katika mtaa wa Manhattan, moja ya migahawa anayoipenda sana.
 Video zilizopigwa wakati wa kisa hicho Jumatano zinamuonyesha Bw Trump akiwasalimia wateja na kuwaambia kwamba atapunguza kodi wanayolipa kwa serikali.
Kwenye video, Bw Trump anaonekana akiwaambia wateja: "Tutapunguza kodi mnayolipa, msiwe na wasiwasi kuhusu hilo."
Kundi la wanahabari waliopewa kazi ya kufuatilia safari za rais huyo mteule, inadaiwa waliambiwa na msemaji wa Bw Trump, Hope Hicks, majira ya saa 18:45 kwamba alikuwa amekamilisha shughuli za siku na kwamba walikuwa huru kwenda nyumbani.
Dakika 45 baadaye, msafara mkubwa wa magari ulionekana ukiondoka kutoka ofisi kuu ya Bw Trump kwa sasa katika jumba la Trump Tower. Msafara huo ulijumuisha magari zaidi ya kumi na gari la kubeba wagonjwa.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.