DOLA MILIONI 25 ZALIPWA NA TRUMP KUMALIZA KESI ILIYOKUWA IKIMKABILI
Wakili wa rais mteule wa Marekani Donald Trump ametatua kesi ya
mamilioni ya madola iliyokuwa inamkabili mteja wake ili apate nafasi ya
kutekeleza majukumu yake mapya na kuangazia changamoto zinazoikabili
Marekani.
Trump alikuwa ameshtakiwa na wanafunzi wa zamani kwa
ubadhirifu wa pesa katika chuo kikuu cha Trump,ambapo wanafunzi walilipa
maelfu ya madola kwa masomo baada ya kuahidiwa kwamba watafunzwa siri
juu ya uwekezaji
Rais huyo mteule amekuwa akikanusha madai hayo
lakini hatimaye ameamua kulipa dola milioni ishirini na tano ili
kumaliza kesi hiyo. Mpango huo hata hivyo haumuhitaji kukiri kwamba
alifanya makosa.
Leave a Comment