CHUO CHA MAKERE UGANDA CHAFUNGWA
Chuo kikuu cha Makerere ( Makerere University ) yenye maskani yake nchini Uganda kimefungwa. Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameamuru chuo hicho kifungwe mara moja kutokana na mgomo unaofanywa na wahadhiri wa chuo hicho.
Chuo kikuu cha Makerere Uganda
Wanafunzi pia wameanza kuondoka chuoni hapo kufuatia tamko hilo lililotolewa na rais Museveni hapo jana majira ya jioni.
Chama cha wahadhiri Jumatatu kiliamua kuendelea na mgomo hadi
wahadhiri walipwe marupurupu ya miezi minane ambayo yamefikia Sh bilioni 32.
Wanafunzi
walijiunga na mgomo Jumanne, na walitaka kukutana na Rais Museveni
badala ya mwenyekiti wa baraza simamizi ya chuo chini ya uenyekiti wa
Dkt Charles.
Naibu chansela wa chuo hicho Prof Ddumba
Ssentamu wiki iliyopita alikuwa amewasihi wahadhiri wakubali kurejea
kazini huku suluhu ya kudumu ikiendelea kutafutwa.
Leave a Comment