BAADHI YA MASHABIKI MAN UNITED WALIJIFICHA CHOONI KUUTAZAMA MTANANGE WA MAN UNITED NA ARSENAL
Mashabiki wawili wa klabu ya
Manchester United waliutumia usiku wa kuamkia mechi kati ya klabu hiyo
na Arsenal katika choo cha uwanja wa timu yao katika juhudi za kutazama
mechi kati ya klabu hizo mbili.
Mashabiki hao walikuwa wametembelea uwanja huo lakini baadaye wakajificha ndani ya choo hicho.
Walipatikana
siku ya Jumamosi alfajiri wakati wa ukaguzi wa kiusalama kabla ya
kukabidhiwa maafisa wa polisi ambao waliamua kutowakamata.
United imesema kuwa hakukuwa na tishio lolote la mashabiki walioingia katika uwanja huo kushabikia mechi hiyo.
Wawili hao walifanyiwa ukaguzi wa kisalama kabla ya kuingia katika uwanja huo kabla ya kuanza ziara yao uwanja huo.
Kisa
hicho kinajiri miezi sita baada ya mechi ya ligi ya premier kati ya
Manchester United na Bournemouth kusimamishwa kwa muda katika uwanja wa
Old Trafford baada ya mfuko uliotuhumiwa kupatikana katika choo
kilichoko katika kona ya uwanja huo.
Hatahivyo ilibainika kwamba kilikuwa kilipuzi bandia kilichowachwa baada ya zoezi mapema wiki hiyo.


Leave a Comment