NUH MZIWANDA AFUNGA NDOA NA MREMBO HUYU , SHILOLE AMTAKIA KHERI NA KUMPA UJUMBE MAALUMU
Wanandoa wapya kama Tunda man na Mabeste inaonekana wametoa motisha kwa wasanii wengine pia kuoa kwani sasa imekuwa ni zamu ya hitmaker wa Jike Shupa Nuh Mziwanda amefunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu anayeitwa Nawal.
Mke wake huyo alipost picha katika mtandao wa instagram akiwa ameshafanyiwa urembo special kwa ajili ya ndoa yake ya Nuh Mziwanda.
Team nzima ya siri za jamii inamtakia Nuh Mziwanda na mkewe Nawal maisha marefu na yenye upendo katika ndoa yao.
Himaanishi watu mkiwa mmetengana ndio mkawekeana vinyongo vya milele lakini inapotokea mwenzio amefanya jambo la kheri kumpongeza ni jambo la busara hii imetokea kwa shilole baada ya kuweka tofauti pembeni na kumpongeza nuh mziwanda katika hatua muhimu alioichukua ya kufunga ndoa.



Leave a Comment