BAADA YA MAN UNITED KUPOKEA KIPIGO UTURUKI - SOMA ALICHOSEMA MOURINHO NA WALICHOANDIKA MAGAZETI MBALIMBALI YA ULAYA JUU YA MCHEZO HUO
Hapo jana miamba ya soka ya Uturuki Fenerbahce iliichapa united kwa mabao mawili kwa moja katika mchezo wa ligi ndogo ya ulaya yaani Europa league.
Ikumbukwe kuwa katika mchezo uliopita united alishinda kwa mabao 4 kwa 1. Hivi sasa Manchester united ameshuka mpaka nafasi ya tatu katika msimamo wa kundi A.
Jose Mourinho amekituhumu kikosi chake kuwa walicheza kama wapo kwenye mechi ya kirafiki.
Mshambuliaji Moussa Sow alifunga kwa kombora la kushangaza la
kupitishia mpira juu ya kichwa, naye Jeremain Lens akaongeza jingine
kupitia frikiki kabla ya Wayne Rooney kufunga bao la kufutia machozi
mechi ikikaribia kumalizika.
Bado lake hilo la dakika ya 89 limemuwezesha kufikia magoli 38 Ulaya na kufikia rekodi ya Ruud van Nistelrooy.
Mourinho amesema: "Matatizo yetu yalianza na mtazamo wetu wa
kiulimwengu. Walikuwa wanacheza fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya,
tulikuwa tunacheza mechi ya kirafiki ya majira ya joto. Huo ndio
uhalisia wa jinsi mechi ilianza.
"Walistahili kushinda, soka
haihusu tu ubora, kuna kutia juhudi pia, kujitolea, kujituma na
kujitolea kabisa. Lazima ucheze dakika zote 90 kwa hamu na umakinifu.
"Katika
mazingira kama haya, kuwapa nafuu wapinzani wako (kwa kufungwa mapema),
hapo ndipo wanataka kuwa. Kisha, tulituliza kasi ya uchezaji na kuanza
kumshinikiza refa, kuigiza kwamba tumechezewa vibaya na hayo ndiyo
makosa yetu."
Meneja huyo wa zamani wa Chelsea hata hivyo alikiri kuwa "moja ya mambo mazuri leo ni kwamba Rooney hatimaye amefunga bao."
Sasa angalia hapa magazeti ya ulaya yalivyochapisha habari za mechi ya jana:





Leave a Comment