ARSENE WENGER: SIJASAHAU ALICHOTUFANYIA MARCUS RASHFORD
Tukielekea kwenye mechi ya Manchester Vs Arsenal kuna habari nyingi
zinatokea. Moja ya habari kubwa ya leo ni kuhusu Wenger alivyomzungumzia
mchezaji Rashford.
Akizungumza kwenye press kuhusu kikosi cha Manchester united,
waandhishi wa habari walikua wana hamu ya kujua maoni ya Wenger kuhusu
kutokuwepo kwa Zlatan. Lakini tofauti ya mategemeo Wenger alisema sema
kwamba kwa Man United hatari haipo kwa Zlatan.
Arsene Wenger asema kwamba hatari ipo kwa kijana wa miaka 19 Marcus Rashford. ,“Tusisahau mwaka jana, kijana aliyetuua ni Rashford”. Kwa sentesi hiyo Wenger alionyesha kwamba wasi wasi wake haukua sana kwa Zlatan zaidi ya Rashford.


Leave a Comment