ANTHONY MARTIAL AUMIZWA KUPOKONYWA JEZI NAMBA 9 NA ZLATAN IBRAHIMOVIC

Mshambuliaji wa Manchester united, Athony Martial mwenye umri wa miaka 20 amechukizwa na kitendo cha kupoteza jezi yenye nambari 9 mgongoni kwa mshambuliaji mkongwe Zlatan Ibrahimovic aliyesajiliwa msimu huu.


Martial alipewa jezi yenye namba 9 baada ya uhamisho wa Euro millioni 36 akitokea timu ya Monaco ya Ufaransa. Alikuwa kipenzi cha kocha aliyepita Louis Van Gaal kwani alikuwa akiwekwa kikosi cha kwanza mara kwa mara. Lakini ameipoteza nafasi hiyo kwa kocha mreno Jose Mourinho.
"Siwezi kudanganya kwenye hili, aliumia sana Manchester United ilipompokonya namba 9 kutoka kwake. Alishangazwa na hilo na alikuwa hana furaha kwa muda" Alisema mshauri wa Anthony Martial, Philipe Lamboley.
"Ni mchezaji mahiri, anaelewa kwamba inabidi aipiginie nafasi yake" aliongeza mshauri huyo
Hivi karibuni kiwango cha mchezaji huyo kimekuwa kikishuka kufuatiwa kupoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester United pia jina lake halikutajwa na kocha wa Timu yake ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps kwenye kikosi cha timu ya taifa kitakachoshiriki mechi za kufuzu kombe la dunia.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.