ALIYEKUWA AKIMKOSOA OBAMA ATEULIWA KUWA WAZIRI WA AFYA NA DONALD TRUMP
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua Tom Price kuwa waziri wa Afya katika serikali yake.
Bw
Price, 62,amekuwa katika Bunge la Congress akiwakilisha jimbo la
Georgia na ni mtaalam wa upasuaji wa mifupa ambaye amekuwa akiongoza
kamati ya bajeti katika Bunge la Wawakilishi.
Atatekeleza jukumu
muhimu katika mipango ya chama cha Republican wa kuubadilisha mpango wa
bima ya afya ulioanzishwa na Rais Obama, ambao hufahamika sana kama
Obamacare.
Wakati wa kampeni Bw Trump aliapa kwamba atabadilisha
sheria hiyo ambayo imekuwa ikitazamwa kama moja ya mambo makuu
aliyoyafanya Bw Obama wakati wa utawala wake.
Lakini amesema kwamba kuna baadhi ya vipengele vya sheria hiyo ambavyo atavihifadhi.


Leave a Comment