ALBUM YANGU YA KIMATAIFA ATAKUWEPO RIHANNA, RICK ROSS..MZIKI UNGEKUWA SAUTI NINGEMSAINI WEMA SEPETU



Ikiwa ni takribani siku moja imepita tangu kundi la muziki wa kizazi kipya lijulikanalo kama WCB kupitia msanii wao Richard mavoko kutoa nyimbo akiwa amemshirikisha mmoja kati ya wasanii wanaofanya vizuri Diamond Platnumz, Siku ya Leo tarehe 23 november 2016, Diamond Platnumz alitembelea studio za clouds fm na kufunguka mambo mengi ikiwa ni pamoja na album yake ya kimataifa kwa kuipa thamani kwa kuwashirikisha nguli wa muziki marekani ikiwa ni pamoja na Rihanna na Rick Ross Pia mbali na hayo amejibu comment ya instagram ailiondikwa na Ommy Dimpoz kwa kusema anafanya mziki wa kiujanja ujanja Diamond Platnumz ameeleza kupitia kipindi cha XXL kinachorushwa Clouds Fm " Mziki wangu unaweza ukawa wa ujanja ujanja lakini natumia akili nyingi kuona namna gani mtu ataipenda nyimbo yangu, Mziki ukitumia sauti pasipo kujua unatunga kitu gani unaonekana unapiga makelele na mziki ungekuwa sauti ningemsaini Wema Sepetu inataka tenzi uandike ujue mtu anataka mziki wa dizaini gani, nyimbo gani na ukiskiliza nyimbo zangu bro maneno yangu yanavyopangiliwa kwa hyo ni tekniki sasa mtu anapokuwa anapaniki na kusema ni mziki wa ujanja ujanja lakini ndio unavuma na wewe kama mwanamuziki mkali mbona mziki wako unaishia kuishi Tanzania tu haufiki nchi zingine ivume Africa nzima tujue kama ni kali show zako ni Tanzania ukipata kenya Maskini ya Mungu mshkaji wako kakuunganisha" hayo ni baadhi ya Maneno aliyozungumza diamond platnzumz na kuongeza kuwa Universal Studio ndio watu watakaosambaza Album yake Duniani.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.