WASANII WA HIP HOP WATANO WENYE PESA NYINGI DUNIANI KWA MUJIBU WA JARIDA LA FORBES
It’s
all about the Benjamiz na bado wanaendelea kuzitaguta hawa jamaa
watano. Wana nguvu sana kwenye muziki wa Hiphop na wametajwa na
forbes.com kwamba ndio wanapesa nyingi kuliko wasanii wengine wote
kwenye muziki wa Hiphop.Kwenye hii story pia utajua connection yao
kwenye sports
Diddy
ameendelea kuongoza list ya wasanii wa Hiphop wenye pesa nyingi
duniani. Vyanzo vya pesa za huyu jamaa ni kutokana na clothing line yake
ya Sean John ambapo hivi sasa ame-launch perfume mpya inatwa 3AM. Brand
ya maji Aquahydrate ambayo yalikua official water ya Manny Pac kwenye
MayPac. Vyanzo vikubwa vya pesa za Diddy ni Ciroc Vodka pamoja na DeLeon
tequila chini ya kampuni yake ya Combs Wines and Spirits akishirikiana
na kampuni kubwa duniani ya vinywaji Diageo.
Diddy
anategemewa kuendelea kupanda juu kwasababu hivi sasa TV network yake
ya Revolt inafanya vizuri sana nab ado ana investment nyingine
mbalimbali kama Blue Flame Angency,Bad Boy Record Label na nyingine
nyingi.
Kwenye
michezo Diddy aliwai kuhusishwa na tetesi za kutaka kuwekeza kwa kiasi
kikubwa kwenye timu ya Crystal Palace wakati ipo ligi kuu.
- Dre – $700 million
Alitegemewa
kuwa bilionea wa kwanza kwenye Hiphop lakini haijawa hivyo. Baada ya
kuuza brand ya Beats by Dre kwa kampuni ya Apple pesa alizopata zimempa
boost ya kufika namba mbili lakini sio juu ya Harlem boy P Diddy.
Lakini
Dr Dre ameweka historia kwa wasanii wa Hiphop kwasababu alipata pay ya
ghafla na kuongeze net worth yake tofauti ya wasanii wengine ambao
ilibidi wasubili miaka kupiga pesa alizokamata Dr Dre.
- Jay Z – $550 million
Jay
Z anatabiliwa kufanya vizuri kwenye miaka ijayo kwasababu ya kuzindua
mtandao wake ambao unafanya kazi ya online streaming ya music unaitwa
Tidal. Uwekezaji wa kwenye internet siku zote huwa unalipa kwa haraka na
kiasi kikubwa sana.
Lakini
pesa hizi za sasa hivi za Jay zinatokana na mgawanyiko wa uwekezaji
chini ya kampuni yake ya Roc Nation. Label yake inawasanii wanaofanya
vizuri sokoni na pia anawekeza kwenye michezo na Roc Nation Sports. Jay Z
anamsimamia wachezaji maarufu kwenye NBA,NFL na michezo mingine kama
MVP wa NBA 2013/2014 Kevin Durant na mchezaji WNBA Skylar Diggins.
Vitu
vingine ni Armand de Brignac Champagne,Club za 40/40 na vitu vingine
mbalimbali. Kwenye michezo Jay Z alihusishwa kuhusu uwekezaji kwenye
club ya Arsenal lakini hivi sasa anategemewa kuwa partner wa David
Beckham kuanzisha timu ya soccer USA.
- 50 Cent – $155 miilion
Kwenye
music 50 Cent hajatoka miaka mingi sana iliyopita ukifanisha na wenzake
ambao wapo kwenye top 5 lakini amefanikiwa ku-make pesa nyingi sana kwa
muda huo mfupi.
Baada
ya kupiga $100 milion baada ya kuuza Vitamin water mwaka 2007, 50 Cent
anategemea kupiga pesa nyingi kwenye uwekezaji wake mpya kutoka kwenye
SMS headphones,Effen Vodka na Frigo underwear.
- Birdman – $100 million
Huyu
jamaa ameshuka kidogo kutoka $160 million kwa mwaka jana hadi hadi
mwaka huu. Pia tetesi za kutaka kuondoka kwa wasanii wakubwa kwenye
label yake kama Lil Wayne inaweza kusababisha akashuka Zaidi mwakani.

Leave a Comment