UNAPENDA TV? PANASONIC WANAKULETEA TV YA KIOO ( INVISIBLE TELEVISION)
Katika maeneo mengi Duniani moja ya vivutio vya Nyumba ni pamoja na Television, katika kuliboresha hilo kampuni ya Panasonic ya Japan imetambulisha Television mpya inayofanana na kioo. Television hiyo bado ipo kwenye maboresho madogo kabla ya kuingia sokoni.
Televisheni ya kioo ya Panasonic
Television hiyo inapowashwa hufanana na Televisheni zingine lakini inapozimwa una uwezo wa kuona mpaka upande wa pili kutokana na hali ya hii Television kuwa ya kioo.
Hapa ni Televisheni hiyo ikiwa imezimwa, una uwezo wa kuona upande wa pili kama inavyoonekana
Panasonic wamewaweka washindani wao katika soko la Televisheni kwa kutoweka wazi tarehe rasmi ya kuanza kupatikana kwa televisheni hizi. Ila inaweza ikachukua muda mrefu kama miaka miwili hadi mitatu kuanza kupatikana sokoni.
Leave a Comment