KISAIKOLOJIA:MWANAMKE WA KUOA NA MANUFAA YA KUWA NAE
Posted by
Jovin Rumanyika
Mwanasaikolojia.
Kuna kasmsemo kanasema kuoa ni kama kununua bidhaa ambayo ujui ndani yake kuna kitu gani , japo kuna njia ambazo ni raisi kutambua kama msichana ulienae ni wa kuoa au sio
Mwanamke anaejua thamani ya mwanaume alienae na kujua maisha ni kama mlima kuna kupanda na kushuka kwamba maisha sio shada la maua yaliopendeza amabayo hayanyauki lazma ajue kuna kupata na kukosa na mnapokosa unafata uvumilivu wa hali ya juu kwa kutambua wewe ni mwenzawake wa maishani haki yake kukupenda, kukuvumilia na kukupa moyo kwa kukuponya vidonda vya roho.
1.HANA TAMAA ZA PESA
Katika maisha ya sasa mwanamke anayependa sana pesa ukikubali awe mkeo mtasumbuana sana. Kwa maana hiyo mwanamke ambaye utagundua hana tamaa ya pesa, kwamba ikiwepo, ikikosekana anabaki kuwa yeye, huyu ni ‘wife material’. Na mwanamke ambae sio mtu wa matumizi mabaya anaweza kufanya mkafikia malengo yenu kama familia na usishangae kwa kusema wewe ni masikini kumbe mwanamke ulienae ndio anaekupa umasikini kwa hyo kufanya chaguo zuri ni jambo la msingi sana.
2.HAYUKO TAYARI KUKUONA HUNA AMANI
Mwanamke ambaye unaona kabisa unapokuwa na matatizo anaumia, anahaha kuhakikisha anakurudisha kwenye hali ya kawaida, kwa kukubembeleza na kukwambia mambo mazuri ambayo yatajurejeshea amani yako uliyoipoteza kwenye maswahibu ya dunia.Laikini unakuta mwingine unarudi nyumbani umechoka anaanza kukufungulia bwawa la maneno kwamba umetoka kwa wanawake zako ambapo ukiachilia mbali matatizo uliyonayo yeye pia ni tatizo katika maisha yako, la msingi ni kujua kila mtu ana nafasi gani katika familia na heshima iwepo.
3.ANAPENDA WATOTO
Utajuaje kama ana mapenzi na watoto? Iko hivi; katika uhusiano wenu ukiona ni mtu wa kupendapenda sana watoto wa marafiki zake, kuwanunulia zawadi, kuwashauri wenzake namna nzuri ya kuwalea watoto, hata akija kupata wa kwake itakuwa ni hivyohivyo. Ukiangalia vijana wengi wa kiume wamekua wakifikiri wanawake walimu ndio walezi wazuri wa watoto lakini pia ukiangalia kiuhalisia ata wanawake ambao wametuzunguka ni walezi wazuri tu wa watoto lakini wengine unakuta ukimuuliza mida ya mchana mwanao yuko api anaweza kukujibu vibaya au kusema ajui, ulezi ni zaidi ya kumzaa mtoto.
4.HESHIMA KWA KILA MTU
Msichana ambaye anaheshimu kila mtu, mdogo na mkubwa, anawapenda na kuwaheshimu ndugu, jamaa na marafiki zako, Japo ndugu wanaweza kuwa wakorofi lakini akatafuta suluhisho na jinsi ya kukueleza kwa heshima, huyu ana sifa ya kuwa mkeo pia. Na pia ni vizuri kuangalia ana ukaribu gani na mama yako mzazi maana katika maisha yetu ya kiswahili kukuta msichana wako anapendwa na mama mkwe ni ngumu kwa hyo maelewano na mzazi wako pia ni jambo zuri.
5.ANAJISHUSHA
Ogopa sana mwanamke ambaye anataka usawa. Anayekufaa ni yule anayejua yeye ni mke, na wewe ni mume. Anayetambua kuwa, mwanaume ndiye kiongozi wa familia, Haijalishi yeye ni nani mahali flani lakini anakuheshimu kama mume na kujua nafasi yake uyo ni mwanamke wa msingi sana kwenye maisha yako.
6.ANAKUONGOZA KWENYE MEMA
Kama mpenzi wako ni wa kukutaka kila siku muende baa au mfanye madili hatari ili mpate pesa, huyu hana sifa ya kuwa mkeo. Mke ni yule ambaye atakuongoza kwenye kutenda mema na kuacha mabaya. Kwa mfano kama unakunywa pombe atakushauri uache, kama siyo mtu wa ibada, atakushawishi umjue Mungu wako japo unaweza usibadilike lakini inakupa imani kubwa.
7.ANAJUA MAISHA NA MAPENZI
Mapenzi yanachukua sehemu kubwa ya maisha ya binadamu. Kwa maana hiyo mwanamke anayekufaa wewe ni yule ambaye anakupenda kwa dhati kabisa lakini pia anajua maisha, lakini wengine hawatambui hilo swala Watu hawa ni wale wanaodhani maisha ni raha tupu na kwamba wanaoishi kwenye shida ni wajinga. Ukweli hauko hivyo, maisha yana changamoto nyingi sana. Kuna siku mambo yanaweza kuwa si mazuri lakini siku nyingine mambo yakawa supa. Mwanamke wa kuoa lazima ajue hivyo.

Leave a Comment