SIRI YA SAKATA LA GERALD PIQUE KUTOA RANGI ZA HISPANIA KATIKA JEZI YAKE
Mnamo October 9, 2016 Mchezaji mahiri wa Barcelona na Timu ya taifa ya Spain aliingia sirini katika headlines za mitandao ya kijamii wakati timu yake ya Taifa ilipokuwa ikichuana na Albania katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu kucheza kombe la dunia 2018 nchini urusi.
Katika mchezo huo Gerald Pique alipewa tuhuma nzito za kutokuwa mzalendo na timu yake ya Taifa kwa kuondoa alama za bendera ya taifa katika jezi yake. Aidha baada ya shutuma hizo mchezaji huyo aliamua kutangaza kutundika daluga kutoichezea timu ya taifa baada ya michuano ya urusi 2018, kwani alihisi Spain haitaki kumuona uwanjani tena.
Mhariri wa makala za AS Mr Alfredo Relano, ambao walihusika na kuzisambaza habari hizi amemuomba radhi mchezaji huyo huku akimtaka aendelee kuitumikia timu yake ya taifa.
Shirikisho la mpira wa miguu la Spain (Royal Spanish Football Federation) nao hawakuwa nyuma kulizungumzia suala hili. Shirikisho hili limetoa tamko kwamba hakuwa Gerald Pique pekee ambaye hakuvaa jezi yenye michirizi ya rangi ya taifa mikononi, hata beki mashuhuri wa Real Madrid Sergio Ramos naye ilikuwa hivyo hivyo na sababu pekee ni kwamba walivaa fulana za mikono mirefu ambazo hazina michirizi hiyo.
Kwa siri kama hizi na siri nyingine nyingi za kisiasa, uchumi, michezo , burudani na mambo ya kijamii usisahau kusubscribe kwenye blogu hii, ku-like page zetu za Instagram na Facebook zinazokwenda kwa jina la "SIRI ZA JAMII"


Leave a Comment