SHERIA:FAHAMU WAKATI WA MAHAKAMA KUBATILISHA UTHIBISHWAJI WA MTEKELEZA MIRATHI AU KUKATAA UTEUZI WAKE

Je, ni wakati gani Mahakama inaweza kubatilisha uthibitishwaji wa Mtekeleza mirathi au kukataa uteuzi wa Msimamizi wa mirathi?
Kifungu namba 49(1) cha Sheria ya Mirathi na Usimamizi wa Mali ya Marehemu,
IJUE SHERIA YA URITHI, MIRATHI NA WOSIA 23 (Probate and Administration of Estate Act,) Sura ya 352 kinaeleza kuwa Mahakama yaweza kubatilisha uthibitishwaji wa mtekelezaji mirathi au kufuta uteuzi wa msimamizi wa mirathi, endapo itabaini yafuatayo;


i. Kwamba mwenendo wa kupata utekelezaji au usimamizi wa mirathi ulikuwa na dosari za msingi,
ii. Kwamba utekelezaji au usimamizi wa mirathi ulipatikana kwa udanganyifu baada ya kutoa mapendekezo ya uwongo au baada ya kuificha mahakama habari muhimu na za msingi katika mirathi hiyo,
iii. Kwamba utekelezaji au usimamizi wa mirathi ulipatikana kwa njia ya malalamiko ya uwongo juu ya jambo la muhimu la kisheria ili kuthibitisha kupatikana kwa utekelezaji au usimamizi wa mirathi, ingawa mlalamiko hayo yalifanywa kwa kutojua au bila nia mbaya,
iv. Kwamba utekelezaji au usimamizi wa mirathi umekuwa hauna maana na haitekelezeki,
v. Kwamba mtu aliyepewa utekelezaji au usimamizi wa mirathi, kwa makusudi ameamua kutopeleka orodha ya mali za marehemu kulingana na sehemu ya kumi na mmoja ( XI) ya Sheria ya Mirathi na Usimamizi wa Mali za Marehemu, Sura ya 352 au chini ya sheria hiyo hiyo, amepeleka mahakamani orodha au taarifa ya uwongo ya mgawanyo wa maliza marehemu. Ikiridhika kwamba mirathi imeendeshwa kinyume na taratibu sahihi zinazoongaza mirathi kisheria na /au kinyume cha masilahi ya warithi, mahakama huwafutia uthibitishwaji au uteuzi, mtekelezaji au msimamizi wa mirathi na badala yake huagiza mtu mwingine ateuliwe na kupewa madaraka ya usimamizi wa mirathi hiyo.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.