SHERIA:FAHAMU HAKI ZAKO UKIWA KAMA RAIA AU MTUHUMIWA WA KOSA LA JINAI
Haki za raia au Mtuhumiwa wa Kosa la Jinai
i. Kila mtuhumiwa wa kosa lolote la jinai anahesabiwa kuwa hana hatia hadi hapo chombo chenye mamlaka (mahakama) ya kuzisikiliza tuhuma kitakapomsikiliza na kumuona na hatia dhidi ya kosa analotuhumiwa.
ii. kila mtuhumiwa ana haki ya kuthaminiwa utu na heshima yake au kutoteswa pale anapotiwa nguvuni;
iii. kila mtuhumiwa ana haki ya kuelezwa kosa alilotenda kabla ya kukamatwa;
iv. kila mtuhumiwa ana haki ya kupewa ushauri wa kisheria;
v. Ana haki ya matibabu pale anapokuwa ameumizwa au anaumwa;
vi. Ana haki ya chakula na malazi;
vii. Ana haki ya kuwasiliana na ndugu zake;
viii. kila mtuhumiwa ana haki ya kukaa kimya mpaka pale anapo hitaji huduma ya kuwakilishwa;
Ruksa ku share na mimi mtazamo wako msomaji wangu kwa kuacha ujumbe wako.


Leave a Comment