SHERIA: SABABU ZA JAMHURI KUENDESHA MASHTAKA YA JINAI YANAPOTOKEA







Posted by
Jackson Msuya
October 8, 2016
Sababu za Jamhuri Kuendesha Mashauri ya Jinai

i. Jamhuri ina dhamana na wajibu wa kuhifadhi na kulinda raia na mali zao dhidi ya wahalifu. Hivyo jamhuri kushughulikia makosa ya jinai ni katika kutimiza wajibu wake huo.


ii. Baadhi ya makosa ya jinai hayana madhara ya moja kwa moja kwa mtu binafsi na hivyo kukosekana kwa mtu ambaye ana nia na yuko tayari kufungua mashitaka dhidi ya mtuhumiwa. Makosa ya aina hii yanajumuisha makosa dhidi ya uvunjifu wa utulivu na amani na makosa dhidi ya maadili mema ya jamii.


iii. Makosa ya jinai ni mazito na yana madhara si tu kwa mtu anayetendewa kosa hilo bali pia kwa jamii nzima.


iv. Makosa ya jinai hujumuisha adhabu ikiwa ni pamoja na kifungo. Mwenye vyombo vya kifungo ni Jamhuri peke yake.


v. Makosa ya jinai yanahitaji gharama kubwa katika kuyachunguza, kuyaendesha na kuwatunza wahalifu pale mahakama inapowatia hatiani na kuwapa adhabu. Hivyo. Chombo chenye uwezo wa kufanya haya yote ni Jamhuri.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.