RAIS MAGUFULI ATOA TAMKO KUHUSU MIKOPO YA WANAFUNZI VYUO VIKUU

Leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa mabweni 20 ya
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye uwezo wa kuchukua
wanafunzi 3,840 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mwezi Juni mwaka
huu wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa maktaba ya kisasa ya
chuo hicho.
Wakati
Rais Magufuli akiweka jiwe la msingi la mradi huo, tayari ujenzi
umefikia asilimia 75 ambapo majengo 20 yaliyounganishwa kimuundo
yamefikia ghorofa ya nne na ujenzi huo unaofanywa na Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA) unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30 Desemba, 2016.
Rais Magufuli ameahidi kuwa, kwa kuwa
majengo hayo yanauwezo wa kubeba ghorofa sita, Serikali itafanya
utaratibu wa kutumia moja ya likizo za wanafunzi kuongeza ghorofa
nyingine mbili ili kuwawezesha wanafunzi wengi zaidi kupata nafasi. Pia Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema..
"Vyuo
vyote vya elimu ya juu viwe na tarehe moja ya kufungua, ukishafungua
kwa haraharaka wakakaa pale kwa mwezi mmoja halafu unawaambia kufanya
usajili lazima walipe wakati bodi haijatoa orodha ya majina ya vijana
watakaokopeshwa, lazima kuwepo na mawasiliano kati ya bodi ya mikopo,
TCU, wizara ya Elimu na wizara ya fedha"
"lengo la
serikali si kuleta usumbufu kwa wanafunzi, lakini ni ukweli pia haitatoa
mkopo kwa wanafunzi wenye uwezo, mtoto wa Ndalichako naye apate mkopo?,
mtoto wa katibu mkuu Kijazi naye apate mkopo? haiwezekani, mkopo huu
umelenga kwa ajili ya kutoa watoto maskini lakini nasikia kule kuna
upendeleo fulani katika kutoa mkopo sasa hili Waziri na bodi
zinazohusike msimamie" John Pombe Magufuli.

Raisi Magufuli akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa hostel ya wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es salaam
![]() |
| Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania TBA Arch. Elius Mwakalinga akitoa ufafanuzi kwa Rais Magufuli kuhusu ujenzi wa Hosteli |
![]() |
| Rais Magufuli akikata utepe kabla ya kuweka jiwe la msingi |

![]() |
Rais Magufuli na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara

ALICHOKIZUNGUMZA RAIS MAGUFULI KUHUSU MIKOPO YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU




Leave a Comment