PAUL LABILE POGBA AWASHIKISHA ADABU UHOLANZI

Hapo usiku wa jana, mataifa mengi yalikuwa uwanjani yakitetea uwepo wao katika kufuzu kombe la dunia nchini Urusi ifikapo mwaka 2018. Moja kati ya michezo iliyovuta hisia za mashabiki wengi ni mechi kati ya uholanzi na ufaransa, ambapo ufaransa walifanikiwa kushinda mchezo huo kwa bao moja pekee lililowekwa kimyani na mchezaji ghali duniani kwa sasa, Paul Labile Pogba wa manchester united.
Kocha wa ufaransa Deschamps, alimtaka Pogba awe mchezeshaji mkubwa wa mchezo huo na amefurahishwa na uwezo mkubwa wa Pobga uwanjani.

 Pogba akishangilia bao lake na wachezaji wenzake, mgongoni ni Raphael Varane na kulia ni Antoine Griezman
Alipoulizwa Pogba juu ya mchezo huu alisema," Najaribu kuzoea, mimi ni mchezaji ninayelenga kusonga mbele zaidi, kocha ananipa maelekezo na ninayafuata kikamilifu"
Goli la Pogba ilikuwa ni combination ya kazi nzuri kati ya beki wa Arsenal Laurent koscienly na kiungo wa West Ham United, Dimitri Payet.
Paul Pogba anakabiliwa na kibarua kizito cha kuikabili liverpool kwenye mechi ya ligi kuu Uingereza juma lijalo.

Kwa siri kama hizi na siri nyingine nyingi za kisiasa, uchumi, michezo , burudani na mambo ya kijamii usisahau kusubscribe kwenye blogu hii, ku-like page zetu za Instagram na Facebook zinazokwenda kwa jina la "SIRI ZA JAMII"

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.