ORODHA KAMILI YA VIJANA WENYE USHAWISHI ZAIDI DUNIANI WA MWAKA 2016
Jarida la Times Magazine wametoa orodha ya vijana wenye ushawishi zaidi duniani. Inatazama athari walio nayo vijana katika vyombo vya habari na katika mitandao.
Orodha hiyo inajumuisha pia waigizaji kutoka vipindi kama Stranger Things, Game of Thrones na Hunger Games.
Ni nyota kutoka sanaa ya musiki, mchezo uanamitindo, sayansi , biashara na siasa. Malala Yousafzai, Jaden Smith, Kylie Jenner, mabinti wa Obama na Chloe
Grace Moretz wote kwa mara nyengine wamejumuishwa katika orodha ya
vijana walio na ushawishi zaidi mwaka huu katika jarida la Times
magazine.
Malala Yousafzai alipigwa risasi na Taliban mnamo 2012.
Tangu hapo amekuwa kijana mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kushinda
tuzo ya Nobel ya amani na kupata kimondo kutajwa kwa jina lake, na kuna
taaifa kwamba huenda kukatengenezwa filamu kuhadithia maisha yake.
Akiwa
na umri wa miaka 19, Malal amejumuishwa katika orodha hiyo ya vijana
wenye ushawishi tangu mwaka 2013 na bado anatetea haki za wasichana
kusoma kote duniani.
Malala Yousafzai
Wengine ni watoto wa Rais wa Marekani Barrack Obama, mama yao pia ni mama anayependwa na wanawake wengi duniani. Ni vizuri kuona kuwa wanafuata nyayo za wazazi wao, huku Sasha
akishirikiana na mamake kuhimiza wanawake wanaelimika Liberia na Mali
naye Malia akitarajiwa hivi karibuni kujiunga na chuo kikuu cha Harvard.
Sasha na Malia Obama
Wakati Kendall na Kylie wote wakitokea mara tatu katika orodha hiyo
ya vijana walio na ushawishi tangu 2013 , mara moja kila mtu kivyake na
mara mbili wakiwa pamoja maarufu "iconic duo," Kendall hakujumuishwa
mwaka huu kwasababu ametimiza miaka 20!
Kylie anepeperusha sifa ya jina la familia Jenner kwa kuorodheshwa kwa mara ya nne sasa.
Awali wakitazamwa kwa sifa ya watu wawili na dadake Kendall, Kylie Jenner mwaka huu amepata sifa peke yake.
Kylie Jenner
Luka Sabbat na Jaden Smith wanawakilisha wanamitindo wanaume wanaosifika.
Katika mtandao wake wa Instagram
anajiita mwanamitindo, mjasiriamali bingwa wa mitindo, na ukampata Tom
Ford kukutumia suti , hapana shaka kuhusu sifa anazojipa.
Na
Jaden hakuachwa nyuma katika suala la mitindo yake ya mavazi
katika siku za nyuma ikiwemo kuonyesha mitindo ya mavazi ya wanawake ya
Louis Vuitton
Luka Sabbat
Anasifika kama mchezaji densi katika kanda ya muziki ya muimbaji
maarufu Sia 'Chandelier na The Greatest', na huambatana na mwanamuziki
huyo asiyejulikana sura katika tamasha kuonyesha mfano wake.
Maddie alijumuishwa pia katika orodha ya mwaka 2015 na akiwana miaka 14 tu ndiye kijana zaidi kutambuliwa mwaka huu 2016.
Maddie Ziegler
Na Orodha hii inakamilika kwa kumalizia na mwanamichezo mahiri Simone Biles. Simone Biles na Laurie Hernandez katika mchezo wa gymnastics
wamejumuishwa pamoja na waogeleaji Katie Ledecky na mkimbiza wa Syria
Yusra Mardini waliong'ara katika mashindnao ya mwaka huu ya Olimpiki.Simone Byles lionyesha umahiri katika
mashindano ya olimpiki ya Rio kiasi cha hatua moja katika mchezo wa
gymnastics kupewa jina lake. na alishinda medali 4 za dhahabu.
Simone Biles







Leave a Comment