MECHI DHIDI YA SOUTHAMPTONI YAMTOKEA MOYES PUANI

Meneja wa klabu ya Sunderland David
Moyes alifukuzwa kutoka eneo wanamokaa Makocha na kulazimishwa kukaa
maeneo ya mashabiki wakati wa mechi dhidi ya Southampton Kombe la EFL
Jumatano usiku.
Sofiane Boufal, aliyenunuliwa £16m, alifunga dakika ya 66 hiyo ikiwa mechi tatu mtawalia Black Cats kushindwa.
Sunderland wameshinda mechi mbili pekee chini ya meneja huyo wa zamani wa Manchester United.
Moyes aliadhibiwa dakika za mwisho mwisho mechi hiyo baada yake kulalamika kwamba klabu yake ilifaa kupewa penalti.
Ombi lake lilikataliwa na mwamuzi wa mechi Chris Kavanagh.

Leave a Comment