MAKOCHA WATAKAOFUATA NYAYO ZA JULIO NA KAIJAGE


Zeben Hernandez - Kocha mkuu Azam


Ligi ya Vodacom Tanzania imezidi kushika kasi na utofauti inaonekana kati ya timu zilizofanya maandalizi ya kweli na zile zilizofanya maandalizi ya zima moto
Hadi kufikia sasa tayari timu 14 zimeshacheza raundi saba za mechi za ligi hiyo na zipo zilizo fanikiwa kuanza vizuri na baadhi mambo yamekuwa magumu hadi kufikia makocha wao kuondolewa kwenye nafasi hizo kwa ajili ya matokeo mabaya.

Mpaka sasa makocha wa timu tatu tofauti wameshaondoshwa kwenye nafasi walizoanza nazo msimu eidha kwa kujiondoa wenye au kufukuzwa na uongozi wa timu kutokana na matokeo mabaya waliyoyapata kwenye mechi zilizopita makocha hao ni Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ wa Mwadui FC ya Shinyanga Peter Mhina wa Majimaji FC na Rogacian Kaijage wa Toto Afrika ya Mwanza.

Makocha hao wamekuwa na sababu mbalimbali zilizosababisha waondolewe kwenye naafasi hizo  Julio akisema Waamuzi wamekuwa wakichezesha kwa maagizo kutoka kwa viongozi wa TFF, Mhina wa Majimaji yeye hajashinda hata mchezo mmoja kati ya michezo sita na ameondolewa na uongozi wa timu hiyo sawa na Kaijage ambaye amejiuzulu mwenyewe baada ya keleleza wanachama na mashabiki wa timu hiyo kutokubali kiwango chake cha ufundishaji.
Baada ya maelezo hayo mafupi Mtandano wa Goal.com unakuletea makocha wengine watano watakao timuliwa msimu huu baada ya Julio na wenzake.

1.Zeben Hernandez
Niwazi kocha huyu Mhispania amekalia kuti kavu kwenye klabu ya Azam FC, baada ya kushindwa kuiipa matokeo mazuri timu hiyo ambayo haipo kwenye kiwango chake cha misimu mitatu iliyopita.
Kupoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya Simba na Ndanda FC,  na sare ya mabao 2-2 dhidi ya Ruvu Shooting, niwazi hakukuwafuraisha wamiliki wa timu hiyo na sasa Hernandezi na jopo lake wanaonekana kutoa visingizio mbalimbali ambavyo kiuhalisia havina ukweli.
Niukweli usiopingika kwamba wamiliki wa timu hiyo hawafuraishwi na mwenendo wa timu yao tangu kuanza msimu huu na endapo matokeo hayo ya vipigo au kutoka sare yataendelea makocha hao wa Hispania wanaweza wasimalize hata mzunguko wa kwanza na kujikuta wakionyeshwa mlango wa kutokea.

2.Kinnah Phiri
Phiri kocha mwenye uzoefu kiasi na ligi ya Vodacom baada ya kujiunga na timu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita na kujionea ushindani, na msimu huu ameanza tangu zoezi la usajili lakini matokeo bado hayajawa mazuri ya kufuraisha kama ilivyokuwa kipindi cha kocha Juma Mwambusi.
Kufanya vibaya kwa timu hiyo yenye milengo ya kuwa bingwa wa ligi ya Vodacom sikumoja kunaweza kuwa sababu ya kutimliwa kwa kocha huyo ambaye, kutokana na aina ya mikakati waliojiwekea viongozi wa timu hiyo inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Kocha huyo ameanza vizuri kwa kushinda mechi mbili na sare moja iliyowafanya kujikusanyia pointi saba na kuongoza ligi katika mechi tatu za awali lakini mamobyamekuwa tofauti na timu hiyo imeonyeshwa kuwa ni yakawaida sana pamoja na usajili wao uliofanywa na Phiri ambao wapo wachezaji aliowasajili kutoka nchini kwake Malawi.
Kama wataendelea kupata matokeo kama hayo anaweza asimalize msimu na kutimuliwa kama ilivyomkuta akiwa na Free State ya Afrika Kusini alipofuzwa baada ya kushindwa kuipa mafanikio timu hiyo.

3.Hans van der Pluij
Tatizo la kufanya mabadiliko ya mapema na kupelekea timu hiyo kupata sare ya kufungana mabao 1-1 na watani zao wa jadi Simba kunaweza kumfukuzisha kazi Mdachi huyo ambaye ameipa mafanikio makubwa timu hiyo tangu alipojiunga nayo miaka mitatu iliyopita.
Pluijm ameanza vibaya kibarua chake msimu huu kiasi cha kuwafanya mabingwa hao watetezi wa ligi ya Vodacom na Kombe la FA kushika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi hiyo licha ya kuwa na michezo pungufu.
Mdachi huyo anadaiwa kufikia mwisho kutokana na kiwango cha timu kinachoonyeshwa kushindwa kwenda na ushindani wa msimu huu jambo ambalo lilichangia kushindwa kutumia vizuri mapungufu ya wapinzani wao Simba waliokuwa pungufu kupata ushindi na kujikuta mchezo huo wakitoka sare ya 1-1.
Inafahamika wazi Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji, huwa hapendi mzaha na amekuwa na maauzi ya kustukiza pindi anapoamua jambo lake hakuna wakumzuia endapo Pluijm atashindwa kurekebisha hali hiyo na timu kuzidi kupata matokeo tofauti na ushindi anaweza kuondolewa kwenye kiti hicho hasa ukizingatia mikakati ya Manji ni kuifanya Yanga kuwa levo za TP Mazembe na klabu kubwa Afrika.

4.Abduli Mingange
Kocha wa Tanzania Prisons ambaye ameanza msimu huu kuifundisha timu hiyo iliyomaliza kwa mafanikio makubwa msimu uliopita ikiwa chini ya kocha Salumu Mayanga aliyekwenda Mtibwa Sugar.
Tangu kuanza kwa msimu huu Prisons haijaonyesha makali yake iliyokuwa nayo msimu uliopita na nimoja ya timu ambayo haina mwenendo mzuri msimu huu, Kocha Mingange ameishusha timu hiyo kwa asili mia kubwa na haijaonyesha kiwango chake ilichokuwa ikikionyesha msimu uliopita.
Kwa mwenendo huo niwazi kwamba Mingange anakazi ya ziada kulinda ajira yake vinginevyo anaweza kuondolewa kwenye benchi la Maafande hao ambao wanashika nafasi za chini kwenye msimamo huku kocha huyo akipata ushindi kwenye mechi mbili tu msimu huu.

5.Malale Hamsini
Huyu ni kocha mpya kwenye ligi ya Vodacom ambaye amejiunga na Maafande wa JKT Ruvu, akitokea timu ya JKU ya Zanzibar ambayo aliipa mafanikio makubwa, lakini tangu kuanza kwa msimu huu timu hiyo haina mwenendo mzuri na inashika nafasi ya 13 kwenye msimamo huku akishinda mchezo mmoja kati ya mechi sita walizocheza.
Malale anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuipa mafanikio timu hiyo angalau kuitoa katika janga la kushuka daraja kama ilivyokuwa misimu miwli iliyopita ambapo ilikuwa chini ya kocha Abdallah Kibaden na Fredy Minziro.
Kwa ushindani wa ligi ya msimu huu, niwazi Malale anakazi ya kufanya kunusuru ajira yake vinginevyo anaweza kurudi Zanzibar kutafuta timu ya kufundisha kwasababu viongozi wa JKT Ruvu hawatokubali kuona timu hiyo ikishuka daraja wakitambua ugumu wa kuirudisha tena ligi ya Vodacom endapo itashuka.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.