MAJIBU YALIOTOLEWA NA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI IVI PUNDE KUHUSU HALI YA KIJANA ALIETOBOLEWA MACHO



uchunguzi wa Macho ya kijana Said maaarufu kama Baba D ambaye alipata mkasa wa kushambuliwa na mtu anayefahamika kwa jina la Scorpion, kisha kutobolewa macho yote mawili hali iliyopelekea kutoona.
Jitida zilizofanywa na Serikali ya mkoa wa Dar es salaam zikiongozwa na mkuu wa mkoa Paul Makonda ili kuweza kumsaidia kijana huyo zilifanikiwa kumfikisha katika Hospitali ya Muhimbili ambako alifanyiwa uchunguzi wa kina ili kujua kama kuna uwezekano wowote wa kumrejeshea uwezo wa kuona.


Majibu ya madaktari yametolewa leo na Mkuu wa Dar es salaam Paul Makonda na kuzua hali ya huzuni kwa Said na familia yake wakiwemo mama mzazi, mama mkwe na mkewe baada ya ripoti ya Madaktari kuonesha kwamba hakuna uwezekano wa aina yoyote ambao unaweza kumfanya kijana huyo akaja kuona tena.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Mkaonda amesema Serikali ya Mkoa itampa Said kiasi cha Shilingi Milioni 10 kwaajili ya kuanzisha biashara itakayomsaidia yeye na familia yake, pia amesema kutakua na gari ambayo itakua ikimsaidia kwenye shughuli zake pamoja na kumsomesha kwenye shule za watu wenye ulemavu wa macho.

side-2
Kijana aliepatwa na janga hilo akiwa na mh Paul Makonda

1 comment:

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.