KILIMO: JE UNAPENDA BIASHARA YA KILIMO? JIKWAMUE KIUCHUMI NA KILIMO CHA VIAZI VITAMU, INGIA SIRINI KUFAHAMU HATUA ZA KUFUATA..

Viazi vitamu ni mojawapo ya mazao ya mizizi ambayo hustawi katika sehemu nyingi nchini na yana sifa ya kustahimili hali ya ukame kama vile ilivyo mihogo.

FURSA:
  • Viazi vitamu hustawi kwenye eneo lenye ukubwa wa wastani
  • Havihitaji mbolea au dawa za mara kwa mara
  • Huweza kuvunwa ndani ya miezi 3-6
  • Hukua wakati wa mvua, pia huvumilia wakati wa ukame


                                                                          Viazi Vitamu


CHANGAMKA:
Ekari 1 ya viazi = magunia 18-20
Gunia 1 ni 80,000/= mpaka 100,000/=
Ndoo 1 ya viazi huuzwa kuanzia 15,000/=
kisado cha viazi huuzwa 3,500/= mpaka 5000/=

FAHAMU:
  • Ukiwekeza 200,000/= faida ni zaidi ya 1,500,000/=
  • Majani ya viazi hutumika kama mboga (Matembele), pia unaweza kuyauza
  • Viazi vyekundu (orange fleshed sweet potato) husaidia kudhibiti kisukari, vina faida kubwa na huuzwa bei kubwa zaidi
JINSI YA KUPIGA MISHE HII:
  • Chagua mbegu zinazovumilia mashambulizi ya wadudu
  • Tengeneza matuta, hii husaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo
  • Ukishapanda palilia kuondoa magugu. Hakikisha pia umefunika viazi vilivyojitokeza ili kuzuia mashambulizi ya fukusi
  • Pandisha udongo kwenye mashina mapema ili kuziba nyufa kabla viazi havijakomaa
  • Wakati wa kuvuna chimbua kwa kutumia jembe. Uangalifu ni muhimu ili kuepuka kukata au kuchubua viazi
  • Hifadhi. Njia bora ni kufukia kwenye mahandaki au kwa kutumia ghala za majani.
Ni fursa nzuri kabisa ambayo vijana tunaweza kuitumia kujikwamua na uchumi na kutatua tatizo la ajira nchini.

Kwa siri kama hizi na siri nyingine kuhusu michezo, burudani, siasa, na masuala ya kijamii usisahau ku-subscribe katika page tovuti hii, pia kufollow na kulike page zetu za Facebook na Instagram zinazokwenda kwa jina la "SIRI ZA JAMII" kwa kuhabarishwa zaidi

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.