INAWEZEKANA KOMBE LA DUNIA LIKAWA NA WASHIRIKI 40 BADALA YA TIMU 32 KAMA ILIVYZOELEKA

Kufuatia maoni yaliyotolewa na wanachama wa baraza la Fifa, Rais wa FIFA Gianni Infantino ana mpango wa kuongeza idadi ya timu zitakazoshiriki kombe la dunia kutoka 32 mpaka 40 au 48.
Mapendekezo hayo yatatolewa katika makao makuu ya Fifa wakati wa mkutano ujao utakaofanyika tarehe 9 mwezi Januari mwaka 2017.

 Ujerumani bingwa mtetezi wa dunia , 2014
Moja ya ahadi za Rais huyu wa Fifa ilikuwa ni kuongeza idadi ya timu zitakazoshiriki kombe la dunia. Mapema mwezi huu raia huyo wa Italy mwenye umri wa miaka 46 alipendekeza kuongeza idadi hiyo hadi 48,huku timu 32 zikishiriki katika awamu ya raundi ya mtoano katika taifa linaloandaa na baadaye washindi kujiunga na timu nyengine 16 katika makundi.
Hata hivyo uamuzi huu umepingwa na baadhi ya wadau wa mpira wakidai utadhoofisha ubora wa kandanda ulimwenguni.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.