FAINALI ZA KLABU BINGWA ULAYA KUANZA KUCHEZWA NJE YA ULAYA
Michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya imekuwa ni kivutio kikubwa
kwa mashabiki wengi wa soka ulimwenguni. Msimu huu pia umeanza na kasi
kali kwa timu mbali mbali kupeana changamoto uwanjani na kuonesha uwezo
wa kutunishiana misuli kwenye kabumbu.
Bingwa Mtetezi wa michuano ya klabu bingwa ulaya Real Madrid, mapema Mei 2016
Katika kuboresha
michuano hiyo, Rais wa Shirikisho la Soka barani ulaya (UEFA),
Aleksander Ceferin raia wa Slovenia amesema bado analifuatilia shauri
lake la kutaka fainali ya michuano hiyo kuchezwa nje ya Ulaya. Rais huyo
amedai kwamba nchi mbali mbali zitatakiwa kutuma maombi ili kuwa
wenyeji katika fainali hizo. Fainali zote 61 zilizochezwa kwa misimu
yote zimechezwa ulaya, hivyo haoni shida ikiwa michuano hiyo ikachezwa
kwenye miji mingine kama New York nchini Marekani au Beijing Nchini
China.
Rais wa Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA), Aleksander Ceferin
Aidha Rais huyo amelenga zaidi kukuza soko la mpira. "Ukiangalia kifedha, hilo haliwezi kufaa. Lakini lazima tufikirie kuhusu
masoko mengine pia. China inavutia kama soko, na Marekani pia. Soka
inaanza kupata umaarufu huko pia," anasema rais huyo



Leave a Comment