FA WAMSHTAKI MOURINHO KWA KUMUINGILIA REFA

Kocha wa Manchester United Jose
Mourinho ameshtakiwa na shirikisho la soka nchini Uingereza FA kwa kudai
kwamba itakuwa vigumu kwa refa Anthony Taylor kusimamia mechi yao dhidi
ya Liverpool.
Mourinho aliongezeawamba kumteua Taylor kusimamia
mechi hiyo ya tarehe 16 Oktoba ilimpatia shinikizo refa huyo mwenye
makao yake Manchester.Mameneja hawaruhusiwa kuzungumzia kuhusu marefa kabla ya mechi.
Mourinho ana hadi Oktoba 31 kujibu shtaka la ukosefu wa nidhamu na kusababisha mechi hiyo kuwa na jina baya.
Taylor alito kadi 4 za njano zote kwa timu ya Manchester United katika sare hiyo ya 0-0

Leave a Comment