EFL CUP: LIVERPOOL YAIGARAGAZA TOTTENHAM, ARSENAL , HULL CITY NA NEWCASTLE ZANG'ARA
Hapo jana tareh 25 October, Nchini uingereza timu kadhaa zilishuka dimbani kuchuana katika kombe la ligi (EFL - English Football League). Katika moja ya michezo iliyosisimua ni mtanange kati ya Liverpool na Tottenham, mchezo huo uliisha kwa Liverpool kushinda bao 2 kwa 1 mabao ya Liverpool yakiwekwa gambani na mchezaji wao Daniel Sturridge na Tottenham wakipata la kufutia machozi kupitia kwa Janssen. Daniel Sturridge ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo huo, sasa amefunga mara 10 katika mechi zake nane zilizopita za kombe la ligi.
Daniel Sturridge akipongezana na wachezaji wenzake katika moja ya magoli aliyofunga
Aidha kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesisitiza kwamba Liverpool haijawa asilimia mia fit bado ina makosa kadhaa ambayo inabidi wayafanyie kazi hivyo awasihi wachezaji wake wasibweteke na matokeo ya hivi karibuni.
Na katika matokeo ya mechi nyingine za jana za kombe la ligi, Arsenal wameigaragaza Reading kwa mabao mawili kwa bila mabao yaliyowekwa wavuni na mchezaji Alex-Oxlade Chamberlain.
Bristol City wamepoteza mchezo wao kwa Hull City kwa mabao 2 kwa 1, nao Leeds na Norwich City katika mchezo wa kukata na shoka walitoka suluhu ya mabao 2 kwa 2 na mchezo huo kuamuliwa kwa penalty ambapo Leeds waliongoza kwa penalty 3 kwa 2.
Nao Newcastle hawakuwa nyuma baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 6 kwa 0 dhidi ya Preston.


Liverpool wapo vizuri sana kuabzia kwenye kiungo na foward na wanaweza kuifunga timu yoyote. Shida iko kwenye defence. Hapo mwalimu lazima afanye kazi ya ziada.
ReplyDelete