DIAMOND PLATNUMZ AMENUNUA MIXER KUBWA WCB AMBAYO TAYARI KASHALIPA ZAIDI YA DOLA ELFU 20
Mkali wa wimbo ‘Salome’ Diamond Platnumz amesema ameagiza mixer kubwa nje ya nchi ili kuboresha studio ya ‘Wasafi Records’ ambayo tayari imeshaanza kushafanya hits kadhaa ambazo zinafanya vizuri katika chart mbalimbali za muziki nchini.Na kwa mujibu wake mixer za aina hyo zinauzwa kwenye record label kubwa aliyasema hayo mbele ya Mh January Makamba na kumalizia kwa kumuonesha video mpya ambayo bado haijatoka ya Diamond platnumz ft Neyo.
Muimbaji huyo wiki hii alitembelewa ofisini kwake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, January Makamba na kumueleza mambo mbalimbali ambayo atayafanya ili kuboresha ofisi hiyo.
“Kwa sasa tunasubiri mixer ifike kwa sababu tuliambiwa hatuwezi kuichukua dukani mpaka tutoe order watutengenezee,” Diamond alimwambia Waziri January. “Zingekuwa ni zile ndogo ndogo wangenipa lakini kwa sababu hii ni kubwa sana lazima utoe order, na tayari nimeshalipia kama dola 20,000 na kitu,”
Pia Waziri January Makamba alimsifia producer wa ‘Wasafi Record’ Lizer kwa kufanya maajabu kwenye wimbo mpya wa Diamond ‘Salome’ ambao kwa sasa unafanya vizuri.

Leave a Comment