DIAMOND PLATINUMZ AMLIPA FADHILA ALIKIBA KWENYE MAHOJIANO NA VIPINDI MBALI MBALI

Kuna uwezekano mkubwa kukawa hakuna bifu kati ya Alikiba na Diamond
lakini wapo wachache wanaokuza hilo jambo kwa maslahi yao binafsi.
Diamond ameonekana kulipa fadhila kwa Alikiba baada ya kumuombea
mashabiki wampigie kura kwenye tuzo ya MTV EMA 2016 akiwa msanii pekee
kutoka Afrika Mashariki anayewania tuzo hiyo.
Kiba atachuana na wasanii wengine wakiwemo Wizkid na Olamide wa
Nigeria na Black Coffee na Cassper Nyovest wa Afrika Kusini huku mshindi
katika hatua ya kwanza ataendelea kwenda kuwania kipengele cha
Worldwide Act: Africa/India ambacho mwaka jana alishinda Diamond
Platnumz.
Akiongea kwenye kipindi cha D’Wikend Chatshow cha Clouds TV, hitmaker
huyo wa Salome amesema, “Nimesikia Alikiba amechaguliwa kwenye tuzo za
MTV EMA. Tufute zile zama za kusema kwasababu wewe unam-support Diamond
ndio huwezi kumpigia kura Alikiba. Akikosa tuzo hiyo haiji kabisa
Tanzania na itaonekana watanzania wote tumeikosa. Kwahiyo tuhakikishe
tuna VOTE ili tuirudishe tuzo hiyo nyumbani.”
Alikiba aliwahi kusema kama hivyo mwezi Juni, mwaka huu kwenye
kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio alipowataka mashabiki
wampigie kura Diamond kwenye tuzo za BET.
Leave a Comment